Jiunge leo

Kilimo Mseto cha Syntropic katika Caatinga

Tabianchi (biome) ya Caatinga ina aina mbalimbali za viumbe hai wenye thamani kubwa waliozoea hasa hali ya hewa ya ukame wa kiasi (semi-arid). Moduli hii inawasilisha mbinu mbalimbali zilizotumiwa na mkulima na mkufunzi wa F4F, Jurandi de Oliveira, kuzalisha chakula na kufuga wanyama, hata kukiwa na kiwango cha mvua cha milimita 236 tu kwa mwaka, bila kutumia umwagiliaji au pembejeo nyingine za nje.

Yale utakayojifunza

  • Jinsi ya kuanza kilimo-mseto katika Caatinga
  • Jinsi ya kujumuisha wanyama katika mifumo ya kilimo-mseto
  • Mtazamo wa jumla (holistic) wa shamba la kijijini
  • Matumizi ya vizuia upepo (windbreaks)
  • Spishi muhimu kwa ajili ya uzalishaji wa chakula cha mifugo
  • Spishi muhimu zilizofaa kwa hali ya hewa ya ukame wa kiasi